Taifa hilo lililofanya jaribio lake la kwanza la nyuklia mwaka 2006 na liko chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kutokana na mipango yake ya kuunda silaha zilizopigwa marufuku, halijawahi kuweka wazi maelezo kuhusu kituo chake cha kurutubisha urani.
Vifaa kama hivyo vinazalisha urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu — ambayo inahitajika kutengeneza vichwa vya nyuklia — kwa kusokota nyenzo hiyo katika mashine pewa kwa kasi kubwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini, Kim alizuru taasisi ya silaha za nyuklia na kituo cha kuzalisha vifaa vya nyuklia vya kiwango cha silaha, bila hata hivyo kutoa maelezo kuhusu eneo wala tarehe ya tukio hilo.
Ujumbe kwa serikali mpya ya Marekani
Kim “alisisitiza haja ya kuongeza zaidi idadi ya mashine pewa ili kuongeza kasi utengenezaji wa silaha za nyuklia kwa ajili ya kujilinda,” vyombo vya habari vya serikali viliripoti, vikichapisha picha za Kim akikagua safu za centrifuges.
Soma pia: Korea Kaskazini yarusha makombora mawili, baada ya nyambizi ya Marekani kuwasili Korea Kusini
Wataalamu wamesema ufichuzi huo wa ghafla wa kituo cha urutubishaji wa urani huenda umekusudiwa kuathiri uchaguzi wa rais wa Marekani mwezi Novemba.
Picha hizo ni “ujumbe kwa utawala ujao kwamba haitawezekana kuiondoa Korea Kaskazini,” Hong Min, mchambuzi mkuu katika Taasisi ya Korea ya Muungano wa Kitaifa, aliiambia AFP.