MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogogolo, leo anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Segerea yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wanchi.
Mkuu wa Wilaya atasililiza kero za wananchi wa kata za Kipawa na Minazi Mirefu.
Katika ziara hiyo DC Mpogolo, ataambatana na wataalamu na wanasheria kutoka ofisi yake na Ikulu waliotumwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wote wenye kero, maoni na ushauri wanaarifiwa kufika na kuonana na DC katika mkutano wa hadhara utakaofanyika saa 9: alasili.