Nyumba 1511 ,viwanda 57 na taasisi 13 zaunganishwa ni mfumo wa gesi asilia -TPDC

Waandishi wa Habari wamekumbushwa kutumia vyema taaluma yao kuisemea Sekta ya mafuta na gesi asilia nchini ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika Uchumi wa Taifa

Kaimu mkurugenzi wa fedha na utawala wa TPDC Bw. Ahmad Massa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bw. Mussa Makame amefungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, leo tarehe 13.09.2024 kuhusu Sekta ya mafuta na gesi asilia jijini Dar es Salaam


Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Bw. Massa amesema “Semina hii iwe sehemu pia ya kujifunza zaidi kuhusu Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga Tanzania (EACOP)mradi ambao umekidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa katika masuala ya mazingira na ustawi wa jamii kwa kuzingatia na kukwepa maeneo yenye vyanzo vya maji, maeneo ya mbuga na hifadhi, maeneo ya kimila na kitamaduni lakini kuepuka kuathiri kwa kiasi kikubwa makazi ya watu pamoja na kuhakikisha jamii zilizopisha mradi zinapata msaada wa chakula, mafunzo ya kilimo na ufugaji, kujengewa nyumba za kisasa zenye mifumo ya uvunaji maji na umeme wa jua na kufungiwa vifaa (inventors) vinavyowezesha matumizi ya vifaa vya kawaida vya umeme”

Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na lengo la kuwajengena uwezo wa kujua Miradi ya kimakakati inayosimamiwa na Shirika hilo.

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu, amesema semina hiyo ni muendelezo wa semina mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Wadau ili kuwajengea uwezo wa kujua Miradi ya kimakakati kwa nchi hasa iliyopo chini ya TPDC.

Serikali inaendelea kutekeleza Miradi mbalimbali ambayo ni pamoja na Mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (LNG), Mradi bomba la kusafirisha mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP), utafutaji wa mafuta Bonde la Eyasi Wembere na Mradi wa utafutaji wa gesi asilia Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini.

kitoa mada juu ya hatua za kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia zinazofanywa na TPDC, Mhandisi mwandamizi idara ya biashara ya mafuta na gesi Bw. Anthony Karomba amesema “tayari jumla ya nyumba 1511 zimeunganishwa na zinatumia gesi asilia nchini kupitia miundombinu iliyojengwa na TPDC katika mikoa ya Dar Es salaam (877), Mtwara (425) na Lindi (209)”.

Related Posts