Mataifa makubwa yaongoze juhudi za amani duniani – DW – 13.09.2024

13 Septemba 2024

Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun, amesema leo Ijumaa kwamba nchi yake itaimarisha ushirikiano wa kijeshi na nchi jirani, na kwamba mataifa makubwa yanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda usalama wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/4kc7M

Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun
Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun.Picha: Florence Lo/REUTERS

Akihutubia kwenye kongamano la kila mwaka la diplomasia ya kijeshi ya China mjini Beijing, Jong Dun amesema China iko tayari kuendelea kukuza mahusiano mazuri na mataifa makubwa ili kudumisha maendeleo thabiti na uhusiano wa kijeshi ili kulinda utulivu wa kimkakati wa kimataifa. 

Soma pia: Rais Xi Jinping wa China ameahidi msaada wa dola bilioni 50 kwa Afrika
Wawakilishi wa  nchi 90 wakiwemo wa mashirika ya kimataifa walihudhuria kongamano hilo la siku tatu linalomalizika kesho Jumamosi.
Ingawa baadhi ya nchi ziliwatuma mawaziri wa ulinzi kwenye kongamano hilo, mataifa ya Magharibi yalituma maafisa wa ngazi za chini.

Related Posts