Dkt Tulia ahitimisha mkutano wa 10 wa wabunge vijana wanachama wa umoja wa mabunge duniani

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson amehitisha rasmi Mkutano wa 10 wa Wabunge Vijana wa IPU uliofanyika Jijini Yerevan nchini Armenia leo tarehe 13 Septemba, 2024.

Dkt Tulia ameeleza umuhimu wa ushirikishwaji wa Vijana katika nyanja zote za maamuzi hususani katika changamoto zinazoikumba Dunia hivi sasa zikiwemo Sera za Elimu na ajira zenye kutoa kipaumbele kwa Vijana.

Aidha, kushirikisha vijana kwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi pamoja na ulinzi na usalama wa Dunia.

Vilevile ameyaasa mabunge kutunga sheria zinazotoa vipaumbele kwa vijana.

Related Posts