MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, Bonnah Kamoli, ameendelea na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja alivyo ahidi na kuwataka wakandarasi kumaliza ujenzi kwa wakati.
Miradi hiyo ni Barabara ya Rozana – Sukita Lata ya Buguruni yenye urefu wa meta 500 ambayo ujenzi wake utagharimu sh. milioni 750 na inajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Southern Link.
Barabara nyingine Faru Iliyopo Kata ya Mnyamani yenye urefu wa metav350 ambayo ujenzi wake utagharimu sh. milioni 499.
Pia Barabara ya Magengeni – KKKT- Kata ya Liwiti, yenye urefu wa meta 500M Ambayo ujenzi wake unagharimu sh.milioni 650.
Bonnah pia alikagua ujenzi wa daraja la Kavesu linalojengwa kwa gharama ya sh.milioni 317.6 na daraja la Kwa Mzava (244.8 ambalo ujenzi wake unagharimu sh milioni 244.8
Mbunge huyo amesema fedha za miradi hiyo zinatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nje ya Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Jiji hilo(DMDP) awamu ya pili.
Ujenzi wa barabara hizo ni wa kiwango cha lami na utaenda sambamba na ujenzi wa mitaro na taa barabarani.
“Tunataka wakandarasi wamalize miradi hii kwa wakati. Wananchi wanacho taka ni kuona barabara zinapitika,”alisema Mbunge Bonnah.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, alisema fedha hizo ni sehemu ya sh.bilioni 10 ambazo Jiji liliingia mikataba na wakandarasi kutekeleza miradi ya barabara na ni mapato ya ndani.