WAHOLANZI WAHITIMISHA MAFUNZO KWA MAAFISA NA ASKARI JKT MBWENI

Afisa Mteule kutoka nchini Uholanzi Rob Van Belkom amepokea tuzo maalumu kutoka kwa Brigedia Jenerali Charles James Ndiege kwenye hafla fupi mara baada ya kufunga mafunzo ya wiki mbili kwa Maafisa na Maaskari yaliyofanyika JKT Mbweni Jijini Dar es Salaam.13,Septemba, 2024.

Kutoka Kulia Afisa Mteule Rob Van Belcom  anayefuata ni  akipokea zawadi maalumu  kutoka kwa mwenyeji wake  Brigedia Jenerali  Charles James Ndiege katika hafla iliyofanyika 13,Septemba, 2024 kwenye Ukumbi wa JKT Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam.

Kutoka Kulia Afisa Mteule Rob Van Belcom  anayefuata ni  Has Feensta  na Sigi Careera a.k.a (Yeba) wakipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika hafla iliyofanyika 13,Septemba, 2024 kwenye Ukumbi wa JKT Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Askari wa JWTZ ambao ni wahitimu wa mafunzo hayo

Wakufunzi hao kutoka nchini Uholanzi  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Askari  wa JWTZ.

Wakufunzi hao kutoka nchini Uholanzi  wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa JWTZ mara baada  ya kufungwa kwa mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa wiki mbili JKT Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv

WAKUFUNZI watatu kutoka nchini Uholanzi ambao wamekuja kwa ajili ya mafunzo kwa Makocha 22 kutoka timu za Majeshi wahitimisha safari yao.

Akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika Septemba 13 2024 JKT Mbweni Jijini Dar es Salaam Brigedia Jenerali Charles James Ndiege amesema shukran za pekee zimuendee Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jacob Mkunda kwa kupitia uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia Conseil International du Sports Military ambao imewaleta wakufunzi hao waliowapa ujuzi Makocha ambao ni Maafisa kutoka Jeshi la Ujamiaji na Magereza walioshiriki mafunzo hayo na Askari kutoka JWTZ.

“Lengo la mafunzo haya kwa Makocha hawa kutoka katika timu zetu za Majeshi nchini ni kuwaaendeleza kimichezo na ili uweze kupata mafanikio yanayoonekana ni vizuri ukapata mafunzo,JWTZ tuna timu nyingi ikiwemo timu ya Mashujaa inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania hivyo haya mafunzo ni kwa ajili ya kuziendeleza timu zetu” amesema Brigedia Jenerali Ndiege.

“Mafunzo haya yameimarisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na nchi ya Uholanzi pia ni matarajio yetu katika siku za usoni huenda tukabadilishana ujuzi zaidi kwa JWTZ kuchukua Askari nchini Uholanzi hii itategemeana na makubaliano na CDF Mkunda” amesema Adisa Mteule Rob Van Belkom.

Belkom ameongeza kwa kusema kuwa anashukuru JWTZ kwa namna walivyo wapa heshima kuba katika kipindi chote cha wiki mbili walizokua nchini na kusifia kupelekwa katika mbuga ya wanyama Mikumi ambapo yeye na wenzake wameshuhudia kwa macho yao kuona wafalme watano wanyama (Big Five Animal) jambo hili limewafurahisha na kuandika historia katika maisha yao.

“Tunaahidi kwenda kuwa mabalozi wazuri wa JWTZ pindi tutakaporudi nchini kwetu” amesema Belcom.

Afisa Mteule kutoka nchini Uholanzi Rob Van Belcom mara baada ya kukabidhi vyeti vya ushiriki wa wahutimu wa mafunzo hayo kwenye Ukumbi wa JKT Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam .

Baadhi ya Askari waliohitimu mafunzo hayo ya ukocha wa michezo yaliyofanyika JKT Mbweni ni ni Ashi Hamis Msangula,Anna David Ngati,Sadiki Abdallah, Adam Isack Mollel, Idd Mohammed Salehe,Amran Abdallah Said,Hussein Uhuru,Mohammed Hussein,Daudi Ramadhan, Emmanuel Joseph Mwijarubi, Francia Kitambala,Athuman Ameir Athuman,Babu Sipendeki Lihundi,Ussi Jeda Haji, Ahmad Abdallah Mashinga na Irene Raphael Kimaro.

Huku Maofisa kutoka Jeshi la Uhamiaji ni Yasin Mussa Kisondo na Ofisa kutoka Jeshi la Magereza ni Patrick John Lumambo.

Wakati huohuo kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo bendi ya muziki wa dansi ya JKT Mbweni a.k.a Wazee wa Jodari imepamba hafla hiyo.

Related Posts