WATANZANIA ASILIMIA 80 KUFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA

 

 

Na. Saidina Msangi, Kibaha, Pwani.

Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau na Taasisi zilizo chini yake imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa Watanzania asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 ili wawezesha wananchi kufahamu umuhimu wa akiba, bima, usimamizi wa fedha binafsi pamoja na kutumia watoa huduma rasmi wa fedha waliosajiliwa.

Hayo yamebainishwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha m, Bw. Stanley Kibakaya, wakati wa kuhitimisha programu ya utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.

Alisema kuwa elimu hiyo ya fedha imepokelewa vizuri na wananchi katika mikoa ya Kagera, Manyara, Singida, Kigoma, Rukwa, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Mtwara, Morogoro, Lindi na mikoa mingine inatarajiwa kufikiwa katika awamu ijayo. 

‘‘Tunafanyia kazi maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa Wizara ya Fedha kuendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi na pia mpango wa sekta ya fedha unalenga kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa wanapochukua mikopo ili kuwawezesha kuondokana na mikopo umiza,’’alisema Bw. Kibakaya.

Alisema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa elimu ya fedha na wananchi wameifurahia na kukiri kuwa elimu hiyo imewasaidia na wataenda kuzitumia huduma rasmi za fedha ikiwemo kuweka akiba, uwekezaji na bima.

Kwa upande wao wananchi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani, wameipongeza Serikali kwa kuwapatia elimu hiyo muhimu ambayo wanaeleza kuwa itawawezesha kujikwamua kiuchumi pamoja na kujiandaa kutumia fursa za uwekezaji katika mifumo rasmi ikiwemo UTT AMIS.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha , Bw. Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa wanapochukua mikopo ili kuwawezesha kuondokana na mikopo umiza pamoja na umuhimu wa kuzingatia mapato na matumizi ili wajiwekee akiba, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.

Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akiwaelekeza wananchi kuhusu mifuko ya uwekezaji inayopatikana katika Mfuko wa Uwekezaji wa UTT Amis na jinsi wanavyoweza kunufaika na fursa za uwekezaji, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha iliyotolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.

Afisa Sheria Mwandamizi Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Ramadhani Myonga, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Pwani, Bi. Grace Tete, akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliohudhuria katika programu ya utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi inayotekelezwa na Wizara ya Fedha, kuhusu mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali, taratibu za kufuata ili kupata mikopo hiyo pamoja na jinsi ya kusajili vikundi na namna ya kuwawezesha kupata fursa ya mikopo husika, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.Baadhi ya wananchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kutoa elimu ya fedha kwa wananchi, kuhusu usimamizi wa fedha binafsi, dhamana za mikopo, riba pamoja na uwekezaji, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.Wananchi wakichangia mada katika majadiliano baada ya mafunzo ya elimu ya fedha kutolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha, walipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya ya fedha kwa wananchi, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Kibaha -Pwani)

Related Posts