Fadlu: Kijili anachangamoto ionayohitaji muda kuisha

IKIWA imesalia saa chache kabla ya Simba kushuka kwenye Uwanja wa Juni 11, jijini Tripoli Libya kuvaana Al Ahli Tripoli, kocha wa kikosi hicho cha Msimbazi, Fadlu Davids amemtaja Kelvin Kijili akisema ni mmoja wa mabeki wa kulia wenye uwezo mkubwa, huku beki huyo akifunguka kwa Mwanaspoti.

Simba ipo ugenini kuanzia saa 2:00 usiku kucheza na Al Ahli katika mechi ya mkondo wa kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku kikosi kikiwa kimekamilika kila eneo kutokana na nyota waliokuwa timu za taifa kuungana na wenzao tayari kwa pambano hilo, lakini Fadlu akimtaja Kijili.

Kijili aliyetua Msimbazi kutoka Singida Big Stars ni miongoni mwa wachezaji wazawa walionekana kujaa kwenye mfumo wa kocha huyo akitumika kipindi cha pili akitokea benchini katika mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu Bara dhidi ya Tabora United na Fountain Gate.

Licha ya beki huyo wa kulia ambaye anajulikana kwa sifa yake ya kuwa na mikimbio hasa anapokuwa uwanjani, kulaumiwa na mashabiki kwa kutokuwa na kutokuwa na mpira mzuri wa mwisho, lakini Fadlu amemkingia kifua akisema licha ya changamoto yake, bado anamwamini na kuamini atakaa sawa tu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fadlu alisema Kijili ni miongoni mwa mabeki wazawa wazuri ila changamoto yake inahitaji muda kwani haiwezi kuisha kwa haraka kama wengi wanavyodhani.

Fadlu alisema, bado ni kijana anayefundishika na muda wote wa mazoezi amekuwa nikimpa mazoezi maalum, hivyo atakuwa sawa.

“Ni beki mzuri sana ila hahitaji presha sana bali maelekezo ya jinsi gani anaweza kufanya ili kuleta mabadiliko ya changamoto yake. Mchezaji hadi anafika Simba ni bora, hivyo tutakapofika nusu msimu, mtamshangaa Kelvin kwa sababu atakuwa na mabadiliko sana,” alisema Fadlu, huku Kijili aliliambia Mwanaspoti kuwa, kocha amekuwa akimpa mafunzo maalumu ili aweze kuwa vizuri zaidi.

Alisema, anafanya sana mazoezi ya kupiga krosi ili awe na mwisho mzuri anapopewa nafasi ya kuwa na mpira.

“Kocha ni kama baba kwetu anafundisha vizuri, muda mwingi ananiambia nitakuwa miongoni mwa mabeki bora katika ligi ya Tanzania. Binafsi nimeanza kuona mabadiliko na ninaahidi kufanya makubwa kutokana na mafunzo ambayo kocha amekuwa akinipatia,” alisem Kijili aliyewahi kutamba akiwa KMC ambaye kwa sasa anacheza nafasi moja na mkongwe Shomari Kapombe na David Kameta ‘Duchu’.

Related Posts