Wananchi waendelea kumuunga mkono viti mwendo Mkaguzi kata Kisangura

Nimwendelezo wa Wananchi kumuunga Mkono Mkaguzi kata ya Kisangura Wilaya Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/Insp Genuine Kimario ambapo wananchi na wadau wenye mapenzi mema wameendelea kuungana na Mkaguzi huyo kwa kutoa viti mwendo.

A/INSP Kimario amebainisha kuwa licha yakuwa na dhamana ya kuhakikisha wananchi hao wako salama na mali zao amewaka wazi kuwa ataendelea kuwashirikisha wadau wa masuala ya Polisi Jamii kuyakumbuka makundi ya wahitaji katika Jamii ili kuendelea kuleta tabasam kwa Wananchi wa kata hiyo.

Mkaguzi huyo ameweka wazi kuwa mwanzo alitoa viti mwendo katani hapo ambapo kupitia mitandao ya kijamii alionekana na wananchi wengine kumtafuta na kumuomba kusapoti kile alichokifanya ambapo wadau wengine wameendelea kutoa viti hivyo kwa ajili ya wananchi wenye changamoto ya viti mwendo.

Aidha ameendelea kuwa shukuru wananchi na wadau wengine ambao wameguswa na kitendo Cha hicho ambapo amewaomba kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya Polisi Jamii.

Vilevile amewaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu kwa Jeshi la Polisi hili kata hiyo iendelee kuwa shwari

Related Posts