Watanzania 9% wanaishi na magonjwa ya kisukari huku asilimia 26 ikiwa ni magonjwa yamoyo

Takwimu za magonjwa yasiyoambukiza ya mwaka 2012 inaonesha watanzania asilimia 9 wanaishi na wagonjwa ya kisukari huku asilimia 26 wana magonjwa ya moyo .

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es salaam Happy Nchimbi Meneja mradi Shirikisho la vyama vya magonjwa Yasiyoambukiza (TANCDA) kwenye semina ya iliyoandaniliwa na TANCDA baina ya waandishi wa habari na Wasanii yenye lengo la kuwapatia elimu juu ya maganjwa yasiyoambukiza

Happy amesema magonjwa hayo yasiyoambukiza kwenye takwimu hizo inaonesha watanzania wengi hawafanyi mazoezi , kutumia vitu vyenye mafuta na sukari pamoja na mtindo wa maisha.

Aidha Happy amesema magonjwa waliyagusia waandishi wa habari na wasanii yasiyoambukiza ni wagonjwa ya kisukari, saratani, magonjwa ya moyo, selimundu magonjwa ya mfumo wa hewa na afya ya akili ambapo amesema elimu hiyo waliyopewa itawasaidia jamii kwa kiasi kikubwa kuelewa magonjwa hayo yasiyoambukiza na kubadili mfumo wa maisha .

Kwa upande wake Dk.Ana Nswila Mshauri wa magonjwa yasiyoambukizwa Shirikisho ka vyama vya magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)amesema magonjwa yasiyoambukizwa yamekuwa ni tatizo kubwa katika nchi hivyo kutokana na tatizo hilo kuna njia mbalimbali za kuweza kuzuia kwa kuwapa watu elimu juu ya magojwa hayo yasiyoambukizwa

Nae Prof.Andrew Swai Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA) amewashauri wananchi kutokutumia vyakula vilivyosindikwa, kutokukoboa nafaka ,kutokuongeza sukari kwenye vyakula mbalimbalimbali.

Aidha miongoni mwa waandishi waliopata elimu hiyo ya magonjwa yasiyoambikiza Kissa Daniel amesema atakuwa mfano wa kuigwa kwa kutoa taarifa kwa jamii juu ya magonjwa yasiyoambukizwa.

Related Posts