WAZEE SAME WAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMAENDELEO MIAKA MITATU YA SAMIA.

NA WILLIUM PAUL, SAME. 

MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amekutana na kufanya kikao na Viongozi wa Baraza na Jumuiya ya Wazee wa Same ambapo kikao hicho kinalenga kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo uliofanyika ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, lakini pia kusikiliza na kutatua kero na malalamiko mbalimbali yanayowakabili Wazee kwenye jamii.

Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same, kikihusisha pia wakuu wa taasisi za Halmashauri hiyo ikiwemo TANESCO, TARURA, RUWASA na SAMWASA wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ambao walipata nafasi ya kuwasilisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakizungumza kwenye kikao hicho Wazee hao pamoja na mambo mengine wameeleza kufurahishwa kwao na kazi nzuri inayofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na usimamizi mzuri wa miradi  ya serikali unaofanywa na serikali wilayani Same.

Aidha wamepongeza pia uwepo wa kikao hicho kwani kimekuwa moja ya sehemu ya kuelewa utekelezaji wa mambo tofauti tofauti yaliyofanyika kwenye jamii zao lakini pia kuweza kupata ufafanuzi sahihi juu ya changamoto zao zinazo wakabili.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Kasilda Mgeni amewashukuru Viongozi wa Wazee hao kujitokeza kwa wingi na kuahidi kuwa ushauri, maoni na changamoto zao walizowasilisha zitafanyiwa kazi kikamilifu ili waendelee kufurahia matunda ya kazi nzuri ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia kwa amani na utulivu.

“Nitumie fursa hii kwaniaba ya wazee wa Same kusema tunakushukuru sana Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo umeendelea kutuletea fedha mbalimbali za miradi ya maendeleo”alisema Kasilda. 

Wakati tukiendelea kufurahia maendeleo haya, ni wakati mzuri sasa kwetu kujipanga kwa ajili ya Chaguzi zilizopo mbele yetu tukianza na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa November 27 kuhakikisha shukrani na pongezi nyingi tunazirejesha kwa Rais wetu kwa haya makubwa aliyotufanyia” Alisema DC Kasilda.

Related Posts