Lunyamila aletewa mtu Mexico | Mwanaspoti

KLABU ya Mazaltan FC inayoshiriki Ligi ya wanawake nchini Mexico, imemtambulisha mshambuliaji raia wa Congo mwenye asili ya Canada, Olga Massombo.

Mshambuliaji huyo amesajiliwa akitokea Gdansk W ya Poland ambako alicheza mechi 21 na kufunga mabao matano.

Inaelezwa Massombo amesajiliwa kuja kuleta ushindani eneo la ushambuliaji ambalo anacheza Mtanzania Enekia Lunyamila aliyetambulishwa hivi karibuni kikosini hapo.

Licha ya ujio wa Mkongamani huyo lakini bado rekodi zinambeba Lunyamila ambaye msimu uliopita akiwa na Eastern Flames alifunga mabao saba kwenye mechi 14.

Tayari Lunyamila amefunga bao moja kwenye mechi tatu alizocheza timu yake ikisalia katika nafasi ya 17 kati ya 18 zinazoshiriki ligi hiyo ikicheza mechi nane na kushinda moja na zilizobaki ni vipigo.

Related Posts