Mbinu zaibeba Simba ugenini | Mwanaspoti

SIMBA imemaliza salama dakika 90 za kwanza za mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho, huku shukrani zikienda kwa mbinu alizozitumia kocha Fadlu Davids za timu hiyo kufunguka mwanzo mwisho ziliipa sare isiyo na mabao mbele ya wenyeji wao, Al Ahli Tripoli ya Libya.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Tripoli (zamani Juni 11) jijini Tripoli Simba ikiwanyima pumzia wenyeji kwa muda mrefu, huku kipa Mousa Camara aking’ara kwa kuokoa michomo kadhaa.

Kocha huyo aliyewaanzisha Abdulrazak Hamza, Yusuf Kagoma na Lionel Ateba katika kikosi cha kwanza, aliinyima nafasi Al Ahli kucheza soka lao la kushambulia kwa kasi kupitia pembeni kwa mipira mirefu, kwani mabeki wa Msimbazi walikuwa na utulivu wa hali ya juu na kumfunika kabisa straika tishio, Mabululu.

Kama kuna idara imeibeba Simba kwenye mchezo huo basi ni safu yao ya ulinzi iliyoundwa na mabeki Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ Che Malone Fondoh, Abdulrazack Hamza na kipa wao Moussa Camara.

Ukuta huo ilifanya kazi kubwa kuzima mashambulizi mengi ya Al Ahli katika mchezo huo ambapo umakini wa mabeki hao ulizima mashambulizi mengi ya wenyeji yakionekana kuwa ya kawaida.

Kwa namna Simba ilivyocheza leo ni kama vile kocha Fadlu alitaka kuimaliza mechi hiyo ugenini, ila umakini mdogo wa eneo la ushambuliaji liliifanya timu hiyo isikamilishe lengo, licha ya eneo la kiungo na mabeki kufanya kazi kubwa kuwazuia wenyeji wasiwapa furaha mashabiki wao waliojazana uwanjani.

Related Posts