Wawekezaji waendelea kumiminika kujionea fursa sekta ya mafuta, gesi na madini

Na Mwandishi Wetu

Kundi la wawekezaji kutoka Umoja wa nchi za kiarabu kupitia kampuni ya AL- SOBAT GROUP wamefika nchini kushirikiana na kampuni ya GSG Energies kuangalia uwekezaji kwenye sekta ya mafuta,gesi Pamoja na madini hapa nchini.

Kwa upande wake afisa wa usimamizi wa dawati la mashariki ya kati Juma Nzima kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania TIC amesema wako tayari kutoa ushirikiano wowote unaohitajika kwa wawekezaji lengo ni kufikia azma ya serikali kuona wawekezaji hawakwamishwi katika miradi yao wanayofanya hapa nchni.

Picha 1.

Afisa Uwekezaji na Msimamizi wa dawati la Mashariki ya kati wa kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)Juma Nzima (kushoto) akisalimiana na ugeni kutoka kampuni ya Al-Sobat Group yenye lengo la kuwekeza katika mafuta na Gesi, Madini, majengo na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GSG Energies, Ismael Elazhari(kulia) Wakati walipowapokea wageni wa Kampuni ya Al-Sobat Group wanaokuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali kwa kushirikiana na GSG Energies,Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Al-Sobat Group,Hisham Hassan na Mohamed Ibrahim.

Picha 2.

Afisa Uwekezaji na Msimamizi wa dawati la Mashariki ya kati wa kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Juma Nzima kushuto akifafnua jambo mbele ya wageni waliowasili Airpot kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GSG Energies, Ismael Elazhari(kulia) Wakati walipowapokea wageni wa Kampuni ya Al-Sobat Group wanaokuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali kwa kushirikiana na GSG Energies,Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Al-Sobat Group,Hisham Hassan na Mohamed Ibrahim.

Kundi hilo la wawekezaji litatembelea maeneo mbalimbali ya nchini ili kujiridhisha na miradi watakayoifanya hapa nchni Pamoja na kukutana na viongozi wa kisekta.

Related Posts