Wakati Ken Gold ikipokea kipigo Cha tatu kwa kupoteza bao 1-0, kocha wa timu hiyo, Fikiri Elias anafikiria kuachia ngazi kuifundisha.
Fikiri ametangaza hilo leo baada ya mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC kumalizika, huku timu yake ikiendelea kusotea ushindi wa kwanza.
Kocha huyo aliyasema hayo wakati akihojiwa na Azam TV, mara baada ya mchezo huo kumalizika akisema ameamua kuchukua uamuzi wa kujitathimini kutokana na kuona mambo kuwa magumu ndani ya timu hiyo.
“Nimeona mambo hayaendi kama ambavyo tulikuwa tunatarajia kabla. Nimeona nichukue uamuzi huo wa kujitathimini kuendelea kuifundisha timu hii,* amesema Fikiri.
“Nachukua uamuzi huu kwa weledi kulinda taaluma yangu. Inawezekana kuna mambo ambayo yanaweza kuisaidia timu kwa hatua nitakayochukua.”
Ken Gold imepoteza mechi zake tatu za kwanza ikiruhusu mabao sita huku ikifunga mabao mawili.