MWANA WA MFALME WA UINGEREZA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MAGOMENI

 

 

Mwana wa Mfalme wa Uingereza (Duchess of Edinburgh) Sophie Hellen Rhys-Jones leo Septemba 17, 2024 ametembelea Kituo cha Afya Magomeni kujionea hali ya utoaji wa huduma za Afya katika kituo hicho.
Bi. Sophie amepokelewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Mohammed Mang’una na kisha kutembelea eneo wanalotoa huduma za Uzazi wa Mpango pamoja na Kituo rafiki kwa huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana. 
Bi. Sophie mchana wa leo anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama pamoja na ujumbe wake wakidajili kuhusu ushirikiano wa pamoja katika kuboresha zaidi huduma za Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.

 

Related Posts