Kihage afurahia utendaji kazi Rusumo

Na Mwandhishi Wetu

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanayakazi katika mpaka wa Rusumo.

Kigahe ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutemebelea mpaka wa Tanzania na Rwanda ( Rusumo ) kwa lengo kuangalia shughuli za Biashara zinazofanyika katika mpaka huo.

Akizungumza wakati wa kujibu taarifa ya utendaji wa kituo hicho kutoka kwa Meneja wa kituo hicho , Kigahe amefurahishwa na utendaji kwa uchapakazi,uadilifu na kujituma kwa watumishi.

“Nimefurahishwa na taarifa ya kutumia muda machache wa kuvusha magari na watu kwa kutumia dk 32 tofauti na upande wa pili wanaotumia muda mwingi” ,Amesema Kigahe.

Meneja wa Kituo cha Forodha cha Rusumo upande wa Tanzania Amosi Illoyo, akielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na mpakani hapo upande wa Tanzania kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara alizotembelea kituo hicho ili kuona shughuli za kibiashara katika mpaka huo.

Aidha amesisitiza kuwa soko la kimkakati la Kahaza linalojengwa litakapoanza kutumika lisaidie wakulima kukusanya mazao toka shambani na kuweka lebo kwenye vufungashio ili kuipa thamani bidhaa yetu kutambulika kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha forodha cha Rusumo, Amos Illoyo amemshukuru Naibu Waziri kwa kufanya ziara kituoni hapo na kuona shughuli za kibiashara zinavyofanyika.

Ameeleza kuwa shughuli zinazofanyika katika mpaka huo ni kukusanya mapato ya serikali ,kuthibiti biashara za magendo zinazofanywa maeneo yanayozunguka mpaka ili kuwezesha ulipaji kodi,na kuzuia bidhaa bandia.

Mpaka wa Tanzania umekuwa ni lango kuu la kupitisha bidhaa kwenda nchi za Rwanda na DR Congo, huku bidhaa zinazopita kwa wingi zikiwamo saruji, vinywaji baridi.

Naye Ofisa Biashara wa Wilaya ya Ngara, Privanus Katinhila amesema kuwa kupitia ziara ya Naibu waziri amejifunza mengi ikiwemo maelekezo aliyopewa ya kujikita kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili kazi yake ifanyike kwa weledi.

Related Posts