Waziri wa Afya wa Lebanon Firas Fabias amethibitisha idadi hiyo ya vifo, ambavyo miongoni mwake ni msichana.
Amesema watu wasiopungua 2,750 wamejeruhiwa na zaidi ya 200 wana hali mbaya kwenye maeneo mbalimbali nchini Lebanon na hasa yanayodhibitiwa na kundi la wanamgambo la Hezbollah.
Wanamgambo wa Hezbollah pia wauawa
Kundi la wanamgambo wa Hezbollah limesema wapiganaji wake wawili pia wameuawa kwenye mkasa huo na wengine wamejeruhiwa nchini Syria ambako pia kumeripotiwa mkasa kama huo, limesema shirika la Haki za Binaadamu la Uingereza, lenye makao yake nchini Syria.
Limesema, watu 14 ambao uraia wao haujulikani wamejeruhiwa mjini Damascus na kwenye maeneo mengine baada ya vifaa hivyo vya mawasiliano vinavyotumiwa na Hezbollah kulipuka.
Chanzo kilicho karibu na Hezbollah kimesema wawakilishi wa ngazi za juu wa kundi hilo pia wamejeruhiwa. Kwenye taarifa yao, Hezbollah wameishutumu Israel kuhusika.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imelaani kile ilichokilezea kama “kitendo cha makusudi na cha hatari kinachofanywa na Israel cha kuusambaza mzozo. Israel bado haijasema chochote juu ya mkasa huo.
Umoja wa Mataifa waelezea wasiwasi kufuatia kisa hicho
Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kitisho cha kusambaa kwa mzozo kati ya Israel na Hezbollah kufuatia kisa hicho cha kulipuka kwa vifaa vya mawasiliano. Msemaji wa umoja huo Stephane Dujarric amesema mjini New York kwamba tukio hili linatokea katika mazingira tete mno na hiyo inatia mashaka makubwa.
Soma pia:Hezbollah yavurumisha makombora dhidi ya Israel
Amesema wanaendelea kufuatilia na hawapuuzi kitisho kilichopo cha kusambaa kwa mzozo.
Gazeti la Marekani la The Wall Street limesema vifaa hivyo vilitoka kwenye shehena ambayo Hezbollah iliipokea hivi karibuni na mamia ya
wapiganaji walikuwa na vifaa kama hivyo, limesema gazeti hilo likimnukuu mwakilishi wa Hezbollah ambaye hakutambulishwa.
Soma pia:Hezbollah yasema wapiganaji wake wawili wameuawa
amesema anadhani vifaa hivyo viliathiriwa na virusi na kusababisha kupata joto kali, lililosababisha kulipuka.
Mashuhuda wamesema mji wa Bei´rut umekumbwa na hamaki kubwa na kumeshuhudiwa magari mengi ya wagonjwa baada ya milipuko. Wizara ya Afya imewatahadharisha watu kutovutumia vifaa hivyo.
Shule zimefungwa kufuatia agizo la Wizara ya Elimu na watu wameombwa kujitokeza kuchagia damu.