DIWANI wa Kata ya Kivukoni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Mhe. Sharik Choughule akiwa kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro hivi karibuni.
Mhe.Sharik amesema amepanda Mlima Kilimanjaro hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza Utalii wa nchi yetu kwa njia mbalimbali.
Mhe.Sharik amewaomba Watanzania popote pale walipo kuhamasisha na kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii ndani na nje ya nchi.