Dar es Salaam. Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema kada wake aliyekuwa meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob maarufu ‘Boni Yai’ amekamatwa na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Mtatiro Kitwinkwi amesema hana taarifa.
Akizungumza na Mwananchi Kamanda Kitwinkwi kuhusu sakata hilo amesema: “Hapana, sina taarifa.”
Taarifa za Jacob kukamatwa, zimeanza kusambaa mitandaoni dakika chache zilizopita leo Jumatano, Septemba 18, 2024 na kwamba amekamatiwa Sinza, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi limemtafuta, Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu ambaye amesema yupo njiani kuelekea Kituo cha Polisi cha Osterbay.
“Ni kweli amekamatwa na polisi waliovalia sare na wengine wamevalia kiraia maeneo ya Sinza. Walikuwa na defender na tuna taarifa kuwa amepelekwa Osterbay polisi na mimi niko njiani nakwenda.”
Endelea kufuatilia Mwananchi