Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) yatoa Taarifa kwa Waombaji wa Mikopo 2024/2025

Na Mtandao Wetu, Mtanzania Digital

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kuwa baadhi ya maombi yao yamebainika kuwa na kasoro zinazohitaji kufanyiwa masahihisho.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Dk. Bill Kiwia, waombaji wote wanahimizwa kuingia kwenye akaunti zao walizotumia kuomba mkopo ili kuona kama wanahitaji kufanya marekebisho yoyote. Alisisitiza kuwa dirisha la masahihisho litafungwa rasmi Septemba 21, 2024 saa 5:59 usiku.

“Tunapenda kuwataarifu waombaji wote kuwa ni muhimu kuhakikisha marekebisho yanayohitajika yanafanywa kabla ya kufungwa kwa dirisha la masahihisho. Baada ya tarehe hiyo, hatua nyingine za uhakiki zitafuata,” alisema Dk. Kiwia.

Aidha, Bodi imeweka wazi kuwa maombi mapya hayatapokelewa kwa kuwa dirisha la maombi lilifungwa rasmi Septemba 14, 2024.

Related Posts