WAKATI winga Mkongomani, Elie Mpanzu, alitarajiwa kutua usiku wa jana nchini ikielezwa kwa ajili ya kumalizana na Simba, inaelezwa mabosi wa Yanga nao wamejitosa kwa nyota huyo.
Hii yote ni safari nzito ya maandalizi ya dirisha dogo na kama ulidhani ni mapema basi umekosea, kwani Watani huko wameshaanza kuliamsha mapema.
Iko hivi. Mwanaspoti iliwahi kuripoti kuwa, winga Mpanzu alikuwa katika mazungumzo na Simba tangu msimu uliopita, lakini dili hilo lilifeli na staa huyo kutimkia Ubelgiji.
Chanzo cha kufeli kwa mchongo huo ulianza kwa viongozi wa AS Vita, timu aliyokuwa aiichezea baada ya kupundua meza dakika za jioni.
Baada ya Yanga kuona Simba imekwama kumpata Mpanzu dirisha kubwa la usajili, na wao wakaona waanze kumfukuzia rasmi ili kupata saini dirisha dogo.
Licha ya watani hao kumfuatilia mchezaji mmoja, Yanga ilienda mbali zaidi na kuweka dau kubwa kuizidi Simba labda huenda staa huyo atawachomolea Wekundu hao waliyokuwa wakimfukuzia kitambo.
Hapo awali Simba iliweke Dola 130,000 na Yanga ikaamua kuizidi na kuweka Dola 150,000 ili kupindua dili la Wekundu hao, hivyo basi unaweza kusema ile kauli ya ubaya ubwela Wanajangwani wameamua kuikamilisha.
Hii yoye inaonyesha jeuri ya pesa ambayo klabu hizi zinazo kwa kugombea mchezaji mmoja, huku dau likiwa si jambo dogo.
Mpanzu aliyekuwa na KRC Genk ya Ubelgiji a liliambia Mwanaspoti na kusema kuwa, ni kweli Yanga imetupa kete ila mambo bado na alikuwa njiani kuja nchini.
“Ni kweli Yanga wamenifuata wakati naendelea na mazungumzo na Simba lakini bado sijaamua maamuzi ya mwisho wapi pa kwenda nakuja huko,” alisema na kuongeza;
“Timu zote zimenitafuta lakini muda wa usajili bado, hivyo nina muda wa kutosha wa kufanya maamuzi.”
Hatua ya Yanga kumgeukia Mpanzu ni baada ya kuona eneo la winga bado haina mchezaji mwenye kiwango wanachohitaji.
Katika nafasi hiyo ya winga ya kulia inachezewa na wachezaji kama Denis Nkane na Maxi Nzengeli.
Huku kushoto, Farid Mussa pekee hivyo ujio wake Mpanzu utaongezxa kitu kikosini, lakini ni kama itaizidi Simba inayoelezwa ipo nafasio nzuri kumnasa mapema.
Kocha Migeul Gamondi amekuwa akitumia sana viungo katika mifumo yake, hata mfungaji bora msimu uliopita alikuwa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki.
Simba na Yanga kwa muda mrefu zimekuwa zikinyang’anyana wachezaji akiwamo Yusuf Kagoma aliyezichonganisha hivi karibuni akitokea Singida FG.