Kesi ya mtoto wa Askofu Sepeku dhidi ya Kanisa la Anglikana kuunguruma leo

Dar es Salaam. Kesi ya Bernardo Sepeku ambaye ni mtoto wa marehemu John Sepeku aliyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es Salaam, inaendelea leo Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi.

Bernado alifungua kesi ya madai mahakamani hapo, akipinga kunyang’anywa zawadi ya kiwanja alichopewa baba yake mwaka 1978 na kanisa hilo.

Pia, anadai alipwe Sh3.72 bilioni ambayo ni fidia ya hasara ya kifedha iliyopatikana kutokana na uvamizi wa mali ya ardhi katika kiwanja hicho.

Mlalamikaji huyo alifungua kesi hiyo ya madai namba 378/2023, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Kanisa Anglikana Tanzania, Askofu Jackson Sostenes wa Dayosisi ya Dar es Salaam pamoja na Kampuni ya Xinrong Plastic Waste Industry Co Ltd.

Katika shauri hilo, mtoto huyo anapinga kunyang’anywa zawadi ya kiwanja namba 2689 chenye ukubwa wa ekari 20 kilichopo Buza, wilayani Temeke ambacho anadai mwaka 1978, waumini na Wakristo wa dayosisi hiyo, walimpa askofu Sepeku kama zawadi.

Kesi hiyo ya madai ilipangwa kusikilizwa leo Alhamisi Septemba 19, 2024 mbele ye Jaji Arafa Msafiri anayesiliza shauri hilo.

Sepeku anatetewa na mawakili wa Bernardo kutoka kampuni ya uwakili ya kampuni ya Diakonus Attorneys, Deogratias Butawantemi na Gwamaka Sekela, huku wajibu maombi wao wanatetewa na wakili Dennis Malamba.

Wakili Butawentemi alidai kuwa wanatarajia kuwa na mashahidi watatu, ambao watatoa ushahidi wao dhidi ya bodi na kampuni hiyo.

Katika kesi hiyo, Bernardo ambaye ni msimamizi wa mirathi ya baba yake, aliwasilisha maombi saba mahakamani hapo,  kwanza anapinga kunyang’anywa zawadi ya kiwanja namba 2689 chenye ukubwa wa ekari 20 kilichopo Buza mtoni, wilayani Temeke ambacho anadai mwaka 1978, waumini na Wakristo wa dayosisi hiyo, walimpa askofu Sepeku kama zawadi.

Pili, anaomba Mahakama hiyo iamuru Bodi ya Wadhamini ya kanisa hilo, Askofu Sosthenes na Kampuni ya Xinrong Plastic Waste Industry Co Ltd kwa pamoja kulipa Sh33 milioni ikiwa ni hasara aliyoipata mlalamikaji kutokanana na uharibifu wa mazao yaliyowekezwa katika shamba lililo ndani ya kiwanja hicho.

Related Posts