WAKATI timu zikiwa zimebakiza michezo miwili zikamilishe michezo 30 ya mzunguko wa pili wa Ligi ya Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), imeonekana ushindani utakuwa kwa timu tano zinazopambana kujinasua zisishuke daraja.
Timu hizo ni KIUT yenye pointi 34, Mgulani JKT (33), Jogoo (33), Crows (32), Chui (29).
Kati ya timu hizo, imeonyesha Chui ndiyo yenye nafasi kubwa ya kupenya kujinasua kushuka daraja kutokana na viporo saba ilivyonavyo.
Nafasi ya timu hiyo kupenya, itaanzia kupewa pointi saba endapo watapoteza michezo saba itakayofanya wapate pointi 35, huku timu hiyo ikiombea zingine zipoteze michezo yake.
Sheria ya matokeo ya mchezo wa kikapu inaeleza, endao timu itashinda itapewa pointi mbili ikifungwa inapata pointi moja.
Timu zilizotinga kucheza hatua ya nane bora ni Dar City yenye pointi 53, UDSM Outsiders (52),Savio (49), Mchenga Star (49), JKT (46), Vijana ‘City Bulls’, (44), Srelio (42) na ABC (41).