TTCL KUENDELEA KUTOA MCHANGO WA MAWASILIANO KUHAKIKISHA WANAFIKISHA HUDUMA KWA WANANCHI NA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATUMIZI.

Mhandisi Cecil Mkomola Francis Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji -TTC akitoa ufafanuzi wa Jambo kwa Waandishi wa habari Jijini Arusha

Mhandisi Cecil Mkomola Francis Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji -TTCL akimpa ufafanuzi Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (Mb) katika Mkutano wa Kimataifa wa TEHAMA na Mawasiliano, (Connect 2 Connect Summit 2024)

Na. Vero Ignatus,Arusha

Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL limesema wanadhamana kubwa ya kutoa huduma ya mawasiliano, kupitia mkongo wa mawasiliano wa Taifa kwani wameendelea kufanya kazi na kuhakikisha kuwa nchi inaongea kwa kuunganishwa mikoa wilaya ambapo jumla ya wilaya 106 zimeunganishwa Tanzania Bara Kati ya wilaya 139,mkongo huo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano na Intaneti.

Hayo yamesemwa na Injinia Cecil Mkomola Francis mkurugenzi wa ufundi na Uendeshaji -TTC katika Mkutano wa Kimataifa wa TEHAMA na Mawasiliano, (Connect 2 Connect Summit 2024)unaotarajiwa kufungwa leo tarehe 19 Septemba, 2024, katika ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha kwamba kazi kubwa waliyonayo kama Shirika ni kutoa mchango mkubwa wa mawasiliano kuhakikisha wanafikisha huduma kwa Wananchi na kupungiza gharama za matumizi.


Aidha Mkomola amesema Kupitia mkutano huo shirika linatarajia kupata fursa ya kubadilishana mawazo na wataalam wa kimataifa kutoka katika kampuni binafsi, za serikali, na wadau wa ICT ambao wanaweza kuwa washirika katika miradi ya baadaye inayotolewa na TTCL ikiwa ni pamoja na huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Vilevile TTCL inaendelea kutoa mchango wa mawasiliano mkongo wa taifa ambao ulianza kutekeleza mwaka 2013 na kuhakikisha mkongo unayojengwa inakuwa na ubora wa hali ya juu kwa lengo la kufikisha huduma kwa Wananchi na kupunguza gharama ambapo Tanzania ni kiunganishi kikuu cha Mawasiliano kwenye ukanda wa nchi za EAC na SADC,

Sambamba na hayo Mkomola amesema Katika mkutano huu TTCL imebeba jukumu la kuwakilisha Tanzania katika sekta ya mawasiliano kwenye jukwaa la Kimataifa, hivyo ushiriki huo umeonyesha dhamira ya serikali ya kuboresha miundombinu ya mawasiliano na kuhamasisha ujumuishaji wa kidijitali nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki

“Tumeunda mkongo huo na nchi jirani za Kenya,Uganda ,Rwanda,Burundi ,Zambia,Malawi na kuna maunganisho yanayoenda kwenye mpaka na Msumbiji na sasa wanaanza kushughulikia maunganisho na nchi ya DRC Congo,kupitia ziwa Tanganyika hadi mji wa Kalemii Nchini DRC pia wanashugulikia maunganisho kwenda kwenye kituo kilichopo baharini hadi Mombasa Nchini Kenya”Alisema

Mkutano huu umehusisha wadau wote wa mawasiliano nchini Tanzania, Somalia nchi za Afrika Mashariki na kusini kwa Afrika,ulifunguliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (Mb) chini ya kauli mbiu ya ‘Meaningful Connectivity’

Related Posts