MABORESHO ZAIDI YANATARAJIWA SEKTA YA ELIMU,WADAU WAFANYA TATHIMINI

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wameanza kufanya tathimini ya maeneo ya vipaumbele katika sekta ya elimu kwa lengo la kuhakikisha maboresho zaidi yanashuhudiwa katika sekta hiyo nchini.

Imeelezwa maboresho hayo yanalenga hasa uendelezaji wa taaluma ya ualimu, kadhalika mpangilio mzuri wa ajira za wanataaluma hao itakayolingana na mahitaji huku ikifafanuliwa baada ya Serikali kutimiza vigezo vilivyopo itanufaika na mradi wa zaidi ya Sh.bilioni 454.04 ambazo zinazotolewa na Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), ambapo kwa sasa ipo katika tathmini kwa kushirikiana na wadau.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha kufanya tathimini kilichofanyika jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Atupele Mwambene katika kikao cha wadau watajadiliana na kufanya mapitio ya tathmini ya vipaumbele vya nchi kuhusu mradi huo.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI ni kwamba tayari kuna kikosi kazi cha pamoja kilichofanya tathmini tangu mwaka 2022 na kuonyesha vipaumbele vya nchi katika sekta ya elimu na wakati akifungua kikao hicho amesisitiza ushirikiano na watalaam kutumia utalaamu wao kwa lengo la kufanikisha malengo ya Serikali katika kuinua sekta ya elimu.

Kwa upande wake Meneja Programu Mwandamizi wa GPE kutoka Ubalozi wa Sweden, Stella Mayenje amesema kupitia mradi huo Tanzania ilinufaika awali kwa kupata Dola za Marekani milioni 84 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh.bilioni 228.3.

Related Posts