Vladimir Putin atembelea kiwanda cha kutengeneza ndege zisizo na rubani

Rais wa Russia Vladimir Putin siku ya Alhamis alitembelea kiwanda cha kutengeneza ndege zisizo na rubani na vifaa vya umeme vya kivita huko St. Petersburg.

Putin ambaye aliongozana na maafisa kadhaa, akiwemo waziri wa ulinzi wa Russia Andrei Belousov, alikagua kiwanda na kuonyeshwa aina tofauti za droni na vitu vingine vinavyotengenezwa.

Putin amesema Alhamis kuwa Russia inaongeza uzalishaji wa droni kwa mara kumi kufikia takriban milioni 1.4 mwaka huu, ili kuhakikisha majeshi ya Russia yanapata ushindi huko Ukraine

Tangu Russia itume maelfu ya wanajeshi ndani ya Ukraine Februari 2022.

Vita hivyo kwa kiasi kikubwa imekuwa ni habari ya mizinga na drone katika ngome ya kilometa 1,000 kwenye uwanja wa wa mapigano unaowahusisha maelfu ya wanajeshi.

Related Posts