FCC YAJIPANGA KUONGEZA UBORA NA UFANISI KUPITIA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WAKE

 

 

Mkurugenzi wa Tafiti, Muungano wa Makampuni, na Utoaji wa Elimu ya Ushindani, Zaituni Kikula akichangia mada katika mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku mbili kwenye hoteli ya Silver Sands Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Tafiti, Muungano wa Makampuni, na Utoaji wa Elimu ya Ushindani, Zaituni Kikula akiwa pamoja na Roberta Feruz Mkuu wa Kitongo cha Mawasiliano Serikalini Tume ya Ushindani FCC wakati mafunzo hayo ya siku mbili yakiendelea kwenye hoteli ya Silver Sands Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Killian Nango kutoka kampuni ya Small Enterprises supplies Development Corporation (SESDC) akitoa mafunzo wa wafanyakazi wa FCC yanayofanyika katika hoteli ya Silver Sands Kunduchi jijini Dar es Salaam

…………..,…

Tume ya Ushindani Nchini (FCC) imesema itaendelea kutoa elimu na mafunzo kwa wafanyakazi wake ili kuongeza ubora na ufanisi katika kazi wanazozifanya.

Hatua hii inalenga kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wake katika kutoa huduma bora na kuendana na mahitaji ya ushindani katika sekta mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tafiti, Muungano wa Makampuni, na Utoaji wa Elimu ya Ushindani, Zaituni Kikula, wakati akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bw. William Erio, katika mafunzo ya siku mbili yanayofanyika kwenye hoteli ya Silver Sands Kunduchi jijini Dar es Salaam leo, Septemba 21, 2024.

“Ni kawaida kwetu kama FCC kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wetu, ambapo tulianza Dodoma na leo tuko Dar es Salaam.

Katika mafunzo haya, tuna malengo mawili makuu: kwanza, ni kujifunza na kuboresha huduma kwa wateja wetu, na pili, ni kujifunza na kuimarisha utamaduni wetu kama FCC,” alisema Zaituni Kikula.

Bi. Kikula alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kupitia upya utaratibu na utamaduni ambao umekuwepo ofisini tangu zamani ili kubaini mapungufu yaliyopo na kuyaboresha. Pia, mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wafanyakazi wapya kupata elimu na ujuzi unaohitajika katika utendaji wao wa kazi.

“Tunahitaji kuweka misingi imara ambayo itafuatwa na wafanyakazi wote na kueleweka vizuri katika utoaji wa huduma. Ili kutoa huduma bora, ni lazima kuwepo na misingi inayotuongoza katika nyanja zote, na kuiishi misingi hiyo ili kutimiza yale ambayo serikali imetutuma kuyatekeleza,” aliongeza Kikula.

Mafunzo haya ni sehemu ya mpango endelevu wa FCC kuhakikisha kuwa wafanyakazi wake wanaendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kiutawala, huku wakidumisha viwango vya juu vya taaluma na maadili katika utoaji wa huduma kwa umma.

Related Posts