DC KARATU AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAKAZI LA MPIGA KURA.

 

Na. Vero Iganatus

Mkuu Wa Wilaya Ya Karatu Mhe. Dadi   Kolimba awataka wanchi wa wilaya ya Karatu kutokeza kujiandikisha katika daftari la wakazi la wapiga kura zoezi ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 11/10/2024 hadi tarehe 20/10/2024. 

Mhe.Kolimba amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa wakazi wa wilaya ya Karatu kwani  litawapa fursa ya kuwachagua viongozi katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka 2024 kwa maendeleo yao na wilaya kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Kolimba amefafanua sifa kuu wananchi wanaopaswa kuwanazo ili kushiriki zoezi la  kujiandikisha ikiwemo. kuwa mtanzania halali, mkazi wa eneno husika, umri usiopungua miaka 18 na pia kuwa na akili timamu.

Related Posts