NEMC YASHINDA TUZO YA "STORIES OF CHANGE" ILIYOTOLEWA NA JAMII FORUMS KWA MWAKA 2024

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshinda tuzo ya ” Stories of change “kipengele cha Taasisi ya Serikali inayohabarisha Umma kwa usahihi na wakati na kuwajibika kwa wananchi katika utatuzi wa kero za kimazingira zinazowakabili kwa mwaka 2024.

Tuzo hiyo imetolewa leo na Jamii Forums katika ukumbi wa Johari Rotana uliopo Jijini Dar es Salaam hafla iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt Immaculate Sware Semesi , Mkurugenzi Mkuu wa Jamii forums Bw.Maxence Melo amesema NEMC imekuwa mstari wa mbele katika kujibu hoja za mitandao ya kijamii inayohusu masuala ya mazingira hali iliyoleta uwajibikaji na ushirikishwaji katika kusimamia na kuhifadhi Mazingira katika jamii.

Amesema Baraza limekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha umma hasa kwa habari za udhibiti wa sauti zilizozidi viwango, udhibiti taka hatarishi pamoja na umuhimu wa kutenganisha taka kutoka kwenye chanzo.

Awali ilielezwa kuwa taarifa zinazoleta mabadiliko kwa jamii kwenye mitandao kwa mwaka 2024 ziliwasilishwa 1800, hivyo kwa Taaisis kupata tuzo ni uwajibikaji uliotukuka.

Hii ni mara ya nne kwa Jamii forums kuandaa tuzo za taarifa zinazoleta mabadiliko katika jamii zilizoandaliwa na Taasisi mbalimbali pamoja na Mashirika ya Umma






Related Posts