Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema maandamano waliyopanga kufanya kesho Septemba 23, 2024 yatakuwepo kama ilivyopangwa huku ikisisitiza kuwa yatakuwa ya amani na maombolezo ya viongozi wao waliotoweka na kuuawa.
Mbowe ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 22, 2024 akizungumza na wanachama wa chama hicho kupitia mdahalo uliofanyika kwenye mtandao wa X (X Space).
Aidha Mbowe amedai kuwa wametoa taarifa Polisi ya kufanyika maandamano hata hivyo hawajajibiwa.
Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa taarifa zaidi