MAANDAMANO CHADEMA: Polisi watanda Ilala Boma kuzuia maandamano ya Chadema

Dar es Salaam. Hali ilivyo asubuhi ya leo   Jumatatu Septemba 23, 2024 eneo la Ilala Boma, jijini Dar es Salaam ambapo Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa wametanda kudhibiti maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yanayolenga kuishinikiza Serikali kuchukua hatua dhidi ya utekaji na upotevu wa watu nchini.

Septemba 11, 2024 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kufanyika maandamano  ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, yakiwemo ya makada wake, lakini Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.

Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu muhimu ya uwajibikaji.

Amesema jambo jingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts