Maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Maji duniani kuanza leo Septemba 23

Mkuu wa wilaya ya Musoma Mh Juma Chikoka amesema katika kuelekea maadhimisho ya siku ya usafiri wa maji duniani yana anza tarehe23 hadi 26 Septemba katika viwanja vya Mkendo ,manispaa ya Musoma mkoani Mtwara maandalizi yake yamekwisha kamilila kwa asilimia 99.

“Kwa asilimia 99 nimeridhishwa na maandalizi haya na nichukue fursa hii kuwakaribisha wananchi wote wa mkoa wa Mara kwenye maonesho haya kujionea na kujifunza kuhusu masuala ya usafiri kwa njia ya maji” Mh Chikoka

“Maadhimisho haya yanatoa fursa kwa wananchi kijifunza juu ya usalama kwa watumiaji wa usafiri wa maji unaotumiwa na asilimia kubwa na wakazi wa Mara ambao pia ni wavuvi na wafanyabiashara hasa kujifunza zaidi fursa na shughuli za kiuchumi zinazofanyika kupitia bahari na maziwa yetu makuu”

Maadhimisho haya ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yanatarajiwa kufunguliwa kesho Jumatatu na Waziri wa miundombinu,mawasiliano na uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Dkt.Khalid Salum.

Kilele kikitarajiwa kuwa tarehe 26 Septemba 2024,mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa uchukuzi Mh.Prof.Makame Mbarawa.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Navigating the future:safety first”

Related Posts