BREAKING: Polisi “Mbowe, Lissu, Lema na wengine tumewakamata, hawajatekwa”

Kamanda wa Kanda Maalum DSM Jumanne Muliro amesema wanawashikilia watu 14 akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman MBOWE, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na Mwenykiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbless Lema.

Kamanda Muliro  amesema hayo mbele ya waandishi wa habari hii leo Septemba 23 tarehe tajwa ya maandamano hayo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.

Septemba 11, CHADEMA katika mkutano wake na vyombo vya habari, walitangaza azma yao ya kufanya maandamano nchi nzima ili kushiriki maandamano, kuishiniza serikali kuchukua hatua baada ya mfululizo wa matukio ya watu kutekwa na kuuawa lakini jeshi la polisi lilitoa onyo kwa viongozi kuacha kuwahamasisha wafuasi wa chama hicho kujihusisha katika uhalifu huo, na yoyote ambaye ataingia  barabarani basi atakabiliwa  kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Related Posts