Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewapongeza wanafunzi walioshinda katika mashindano ya wanasayansi vijana marufu Young Scientists Tanzania (YST) kwani yanasaidia kupata teknolojia ambazo zitatumika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa tuzo kwa washindi wa YST Profesa Mkumbo amesema kupitia mashindano hayo vijana wamekuwa wanatafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili Jamii katika maisha ya kila siku.
“Kupitia mashindano haya YST inaangalia kutafuta ufumbuzi wa kuangalia namna ya kutafuta suluhisho kuhusu teknolojia kwa maisha ya baadae,”amesema Profesa Mkumbo.
Pia amesema hata tuzo ya YST Mwaka 2024 ni matokeo ya maendeleo ya utafiti ya wanafunzi wa sekondari nchini kwa kuweka mawazo ya umakini wa kujituma katika Uhandisi wa teknolojia ya Sayansi na Hesabu nje ya maisha ya darasani.
Aidha amesema kuwa matokeo hayo hayajatokea bila Serikali kuweka mikakati yake katika uwekezaji wa shule za sekondari na kuendelea kuimarishwa kwa miundombinu ,rasiliamali watu ili kupata matokea zaidi kwa baadae
Hata hivyo amesema Taasisi ya YST imeweka mikakati kuisaidia Serikali Kwa shule za Sekondari katika Sayansi ya Uhandisi wa Teknolojia pamoja na hesabu.