Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka akiwakilisha mada wakati wa mkutano wa kimataifa wa Maafisa Mawasiliano ya Umma Afrika Mashariki unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania, Arusha
Na.Mwandishi Wetu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, leo Jumanne tarehe 24 Septemba, amewasilisha mada katika Mkutano wa kimataifa wa Maafisa Mawasiliano ya Umma, Afrika Mashariki unaofanyika kwa mara ya kwanza Arusha Tanzania.
Prof. Kusiluka amewasilisha mada kuhusu Mawasiliano ya kisanyansi “ Science Communication” akiwataka Maafisa Mawasiliano na Waandishi wa habari kuongeza juhudi kuandika habari na matokeo ya tafiti za kisayansi kwa maendeleo mapana ya Afrika.
Amesema, kufuatia mabadiliko ya Nne ya Kiuchumi duniani yanayoendana na uwekezaji Mkubwa wa katika ubunifu wa kisayansi, Vyombo vya habari na Maafisa Mawasiliano wanaowajibu mkubwa wa kusaidia Afrika na hasa Afrika Mashariki, kuandika matokeo ya utafiti na bunifu za kisayansi zinazofanywa na wanasayansi, ili kuongeza uelewa wa wananchi katika masuala ya Sayansi na kuongeza ushiriki wao katika kuleta mabadiliko chanya.
Amehidi Chuo Kikuu cha Dodoma, kuanzisha mafunzo ya muda mfupi yatakayosaidia waandishi na Maafisa Habari kuandika habari za kisayansi kwa manufaa mapana ya Taifa.
Mkutano huo wa siku tano unahusisha washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Burundi, Rwanda na Sudan; na unajadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeo na Ustawi wa Tasnia ya Mawasiliano ya Umma na Mawasiliano.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka(wa kwanza kushoto) akiwa kwenye mjadala kuhusu Mawasiliano ya kisayansi kwenye Mkutano wa kimataifa wa Maafisa Mawasiliano ya Umma Afrika Mashariki, unaendelea Arusha. Anayefuatia ni Bi. Mildred Mugambi, Afisa Mawasiliano ya Umma kutoka Kenya
Wakiwa kwenye picha ya pamoja ni washiriki wa mjadala kuhusu Mawasiliano ya kisayansi wakati wa mkutano wa Kimataifa wa Maafisa Mawasiliano kwa Umma unaoendea Arusha
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Maafisa Mawasiliano kwa Umma Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini uwasilishaji mada wakati wa mkutano .
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka akiwakilisha mada wakati wa mkutano wa kimataifa wa Maafisa Mawasiliano ya Umma Afrika Mashariki unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania, Arusha