Wamarekani kuwekeza kwa vijana kikapu

SHIRIKISHO la Kikapu Tanzania (TBF) na Taasisi ya Kimataifa ya iCARRe Foundation kutoka Marekani zimeingia mkataba wa miaka miwili utakaosimamia maendeleo ya kikapu kwa vijana.

Hafla hiyo hiyo ilifanyika katika Kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK Park), ikishuhudiwa na makocha wa timu ya taifa na viongozi wa TBF.

Viongozi wa iCARRe Foundatiom waliwakilishwa na mkurugenzi msaidizi, Kristen Bryant aliyeambatana na mkurugenzi mkuu wa tawi la Tanzania, Richard Mtambo.

Mtambo alisema wanategemea kutoa vifaa vya mchezo na mafunzo kwa makocha na viongozi  wa kikapu nchini.

Alisema katika ushirikiano huo watahakikisha timu za Tanzania zinafanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

“Dhamira yetu ni kuona kwa miaka miwili Tanzania inafanya vizuri kimataifa,” alisema Mtambo.

Katibu mkuu wa TBF, Mwenze Kabinda alisema ushirikiano huo utawapa nafasi vijana kujifunza kwa kutumia pia teknojia sahihi na masuala ya usalama na afya ya akili mchezoni.

Related Posts