Makisio ya ukuaji wa Uchumia 2024 yaongezeka – DW – 02.05.2024

Ripoti iliyochapishwa jana na jumuiya hiyo inaonesha kwamba uchumi utakuwa kwa asilimia 3.1 mwaka huu kutoka ukuwaji wa asilimia 2.9 ilivyokuwa mwezi Februari, licha ya changamoto kadhaa kwenye siasa za kilimwengu.

Msemaji wa OECD, Clare Lombardelli, alisema kwamba kiwango cha uchumi kufufuka upya vinatafautiaa kati ya eneo ya eneo, hasa baada ya majanga ya virusi vya korona na vita vinavyondelea sasa Ukraine na Ukanda wa Gaza.

Uchumi wa Marekani ambao ndio mkubwa kabisa duniani unatazamiwa kupanda kwa asilimia 2.6 kwenye mwaka huu, kutoka makisio ya awali ya asilimia 2.1, ukiwa na kasi zaidi ya asilimia 2.5 ilivyokuwa mwaka jana.

OECD pia imepandisha makisio yake kwa taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani, yaani China, ambayo itapanda hadi asilimia 4.9 kutoka makisio ya awali ya asilimia 4.7.

Soma pia:EU yatangaza kuipa Lebanon msaada wa euro bilioni 1

Hali ni mbaya kwenye ukanda wa sarafu ya euro, ambako makisio ni ukuwaji wa asilimia 0.7 tu, tafauti ndogo ya makisio ya asilimia 0.6 iliyokuwa imetolewa hapo kabla.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa ukuwaji wa hadi asilimia 1.5 kwa mwaka 2025, ikilinganishwa na asilimia 1.3 kwa mwezi Februari.

Katibu Mkuu wa OECD, Mathias Cormann, alisema “Uchumi wa dunia umethibitisha kuwa himilivu, kiwango cha kuporomoka kimepunguwa kwa mujibu wa malengo ya benki kuu, na kitisho kwenye muonekano wa uchumi kinazidi kudhibitiwa.” 

Hatua za kibenki kuokoa uchumi

Benki kuu duniani kote zilipandisha viwango vya riba katika jitihada za kukabiliana na kitisho kushuka kwa uchumi, ambacho kilitokana na athari za janga la UVIKO-19 na kuchochewa zaidi na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mwaka 2022.

Benki Kuu ya Marekani na ile ya Ulaya zilizuwia viwango vyao vya riba na masoko yanatarajia sasa kupata magawiyo yao katika miezi ijayo kwani sasa hatari ya kushuka thamani imedhibitiwa.

Rais wa Benki Kuu ya Ulaya Christine Lagarde
Rais wa Benki Kuu ya Ulaya Christine LagardePicha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo, Benki Kuu ya Marekani itazamiwa kupata gawio lake baadaye zaidi kuliko ilivyotazamiwa mwanzoni kutokana na uhimilivu wa uchumki wa nchi hiyo na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.

Soma pia:Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck awasili Ukraine

OECD ilionya kwamba migogoro ya kilimwengu, hasa ule wa Mashariki ya Kati, inaweza kuharibu masoko ya nishati na ya fedha na hivyo kupelekea kupanda tena kwa mfumuko wa maisha.

Kwa hilo, Katibu Mkuu wa OECD, Mathias Cormann, alisema kwamba lazima pawemo na hatua za kisera kuhakikisha utulivu wa chumi ndogo ndogo na kuimarisha uwezo wa chumi za kati.

Uthabiti wa sera za kifedha

Kwa mujibu wa Cormann, sera za kifedha lazima zisalie makini, zikiwa na uwezekano wa kuanzisha riba za kiwango cha chini wakati huu mfumuko ukishuka ili kuvutia ubunifu, uwekezaji na fursa kwenye soko la ajira, hasa kwa wanawake, vijana na wafanyakazi wenye umri mkubwa.

Ripoti hiyo ya OECD ilisema kwamba kuimarika kwa uchumi kwenye familia moja moja, masoko ya ajira imara na makato ya viwango vya riba ni mambo yatakayosaidia kuleta matokeo chanya kwenye uchumi.

Soma pia:Viongozi wa Umoja wa Ulaya kujadili kuhusu uhamiaji na uchumi

OECD imepunguza makisio yake kwa Ujerumani kwa mwaka 2024, hadi asilimia 0.2 kutoka 0.3.

Ulaya kuipatia Ukraine msaada wa euro milioni mia tano

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Ufaransa, iliyo ya pili kwa uchumi mkubwa baada ya Ujerumani katika ukanda wa sarafu ya euro, itakuwa kwa asilimia 0.7 badala ya 0.6 kama ilivyokisiwa awali. Uingereza kwa upande wake, itakuwa na ukuwaji wa asilimia 0.4 kwa mwaka 2024 na 1.0 kwa mwaka 2025, ikiwa kasi ndogo ya vile ilivyokisiwa mwezi Februari.

Related Posts