KESI MPYA YA UBAKAJI YAMKUTA DIDDY – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mwanamuziki wa Hip-hop Sean Combs maarufu kama ‘Diddy’ akiwa bado yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi huku akisubiri kufikishwa Mahakamani kutokana na mashtaka yanayomkabili ya kula njama, kuendesha biashara ya ngono na uhalifu mwingine ikiwemo usafirishaji wa binadamu kwa njia haramu imeibuka tena kesi mpya inayomhusisha Thalia Graves anayedai alibakwa na msanii huyo.

Thalia Graves amedai kuwa Diddy na mlinzi wake walimpa dawa za kulevya kisha kumfunga na kumbaka mnamo 2001 huku wakirekodi tukio hilo katika studio zake za Bad boy.

Graves anasema aliogopa kuripoti tukio hilo kwa kuhofia juu ya usalama wa maisha yake, na ametumia nguvu kubwa kukabiliana na hali hiyo ikiwemo ushauri wa kisaikolojia mpaka kuwa sawa kwani alitamani kujitoa uhai.

Related Posts