KOCHA MPYA WA SIMBA QUEENS HUYU HAPA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Simba imemtangaza kocha Yussif Basigi kuwa kocha mkuu wa timu ya Wanawake ya Simba Queens akichukua nafasi ya kocha Juma Mgunda ambaye ameondoka katika timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

 

 

 

Basigi raia wa Ghana mwenye umri wa maiaka 52 anajiunga na Simba Queens akitokea timu ya Hasaacas Ladies ya Ghana, chini ya uongozi wa Basigi, Hasaacas Ladies imefanikiwa kushinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Ghana.

 

 

 

Mwaka 2021, Basigi aliiwezesha Hasaacas Ladies kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake.

Related Posts