Rais Samia ateua wenyeviti wa bodi sita

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan jana Jumatano Septemba 25, 2024 amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi sita.

Taarifa za uteuzi huo zimetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusiluka, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i. David Chimbi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL);

ii. Balozi Aziz Mlima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO);

iii. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania;

iv. Balozi Valentino Longino Mowola, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano (UCSAF);

V. Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO); na

vi. Profesa Neema Mori ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kipindi cha pili.

Related Posts