Serikali imeendelea kuchukua hatua kadhaa ili kukibidhaisha Kiswahili

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua kadhaa ili kukibidhaisha Kiswahili ambapo Moja ya hatua hizo ni kuandaa Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo leo September 25 2024 wakati akifunga mafunzo ya waandishi waendesha ofisi Mkoani Morogoro ambapo aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Methusela Ntoda

Mhe Mwinjuma amesema kuwa Mkakati huo una lengo la kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa kwa kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kwa rasilimaliwatu wanaojihusisha na lugha hii pamoja na watoa huduma za Kiswahili.

Miongoni mwa mambo yanayolengwa katika mkakati huo ni kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hivyo, kwa kutambua umuhimu wa waandishi waendesha ofisi na kwa kuzingatia maelekezo ya Waziri Mkuu, wamewapa kipaumbele kwa kuanza kutoa mafunzo hayo na ameahidi kuwa mafunzo yatakuwa endelevu kwa maana kwamba yatakuwa yanatolewa kila mwaka mara moja.

Aidha Mhe Mwinjuma ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha nyaraka za serikali na mawasiliano kati ya ofisi moja na nyingine yanazingaz¡tia matumuzi mazuri ya lugha na hivyo kufanya Tanzania idhihirishe kwa vitendo kuwa ni kinara wa Kiswahili.

Related Posts