Vijana wanaongoza kuharibu lugha ya Kiswahili-BAKITA

Baraza la kishwahili Tanzania (BAKITA) limesema vijana ndio wanaoongoza Kwa kuharibu maneno ya kiswahili sanifu kwa kutumia maneno ya mtaani.

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa Baraza la kiswahili Tanzania (BAKITA) wakati wa mafunzo Kwa waandishi waendesha ofisi zaidi ya mia sita yaliyofanyika mjini Moroogoro yenye lengo la kufundisha matumizi ya kiswahili sanifu na fasaha kwenye uandishi.

Amesema mpango wa Serikali ni kuipeleka lugha ya kishwahili kimataifa hivyo hivyo wameanza kutoa mafunzo kwenye Kila kundi ili kuacha kutumia maneno ya yasiyofaa katika jamii hasa vijana ambao wanatumia maneno ya mtaani ambayo hayapo kwenye kamusi.

Naye Mchunguzi Mkuu BAKITA Dokta Rizati Mmary amesema mafunzo hayo yameanza kuzaa matunda kwani taasisi mbalimbali zimekuwa zikipeleka waandishi wao ili kujifunza matumizi ya lugha ya kiswahili sanifu na fasaha.

Akifunga mafunzo hayo naibu waziri wa Wizara ya Utamaduni sanaa na michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma amesema muendelezo wa mafunzo hayo ni kutekeleza maagizo ya Mhe. Waziri mkuu .

Amesema ni wakati Sasa wakuhakikisha lugha ya kishwahili inakuwa kimataifa hivyo mpango huo utasaidia kukuza na kuleta matokea mazuri.

 

Related Posts