WASICHANA ZAIDI YA 4000 WAOKOLEWA KWENYE UKEKETAJI NA NDOA ZA UTOTONI TARIME

 

 Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

IMEELEZWA kuwa zaidi ya watoto 4000 wameokolewa kutoka ndoa za Utotoni na ukeketaji mkoani Mara Wilaya ya Tarime nchini Tanzania kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2006 mpaka sasa hali inayotishia afya za mabinti na mstakabali wa mmaisha yao

Shirika linalopinga Ukeketaji  la Terminationof Female Genital  Mutilation(ATFGM) Wilayani Tarime Mkoani Mara limesema kuwa wanasiasa wanaonekana kuwa chanzo kikubwa cha uwepo wa ndoa za utotoni na ukeketaji kwa wilaya hiyo kwa kushindwa kuyaongea kwa jamii kwa lengo la kulinda nafasi zao.

Pia limesema kwa miaka ya uchaguzi mara nyingi  kumekuwa na ongezeko la wahanga  wengi wanaopitia masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni kutokana na wanasiasa kuyafumbia macho masuala hayo kwa kulinda kura zao.

Akizungumza jana mkoani humo wilayani Tarime ,Meneja Miradi wa ATFGM,Valerian Mgani wakati wa Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni  Tanzania (TECMN) walipofanya ziara katika Kituo chao kinachopokea wahanga wa ukeketaji na ndoa za utotoni kutoka maeneo mbalimbali ambapo wasichana hao ukimbilia mahali hapo kama sehemu ya kujiokoa na matukio hayo kutopata.

Mgani alisema wanasiasa kuyafumbia macho mambo hayo yanakuwa sababu yankuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa wilaya hiyo.

“Suala la siasa  limekuwa ni changamoto wanasiasa karibu wote hakuna ambaye anaweza kusimama jukwaani na kuongea masuala haya yav kupinga ndoa za utotoni wala suala la ukeketaji,wanasiasa wengi huku wameshajichukulia wakitaka wachaguliwe na kuendelea kuwepo katika madaraka ni lazima yeye aweze kuwa upande wa wananchi hasa katika upande wa kutetea masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni.

“Kila mwaka wa uchaguzi kumekuwa na changamoto hii kuwa kubwa ,Mfano mwaka 2020 kumekuwa na changamoto kubwa ya  idadi ya watoto kukimbilia katika kituo hicho kutokana na wengi kutaka kukeketwa na wengine kuozeshwa wakiwa na umri mdogo na hii inatokana na watu kuwa bize na masuala ya siasa  na kushindwa kuwatetea watoto,”alisema.

Alisema kwa mwaka huu hali hiyo imeanza kuonekana mapema hivyo wao kama asasi na kituo wanategemea kupokea wahanga wa masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni zaidi ya watoto700 kituoni hapo.

“Tumejipanga kuwapokea  wahanga wa ukeketaji na hao watoto wanaoozeshwa kwa umri mdogo na pia tumejipanga kufatilia maeneo ambayo yameanza kufanya vitendo hivyo kwa ukaribu zaidi,”alisema.

Mgani alisema serikali inahitaji kuweka nguvu nyingine ya ziada hasa kwa wanasiasa kuwasaidia watoto hao wa kike wanaposimama majukwaani waweze kuongea masuala ya  kupinga mambo ya ukeketaji na kupinga ndoa za utotoni.

Alisema wahanga namba moja ni katika matukio hayo ni wale watoto waliomaliza tayari darasa la saba na suala la  biashara kwa wazee wa kimila na Ngariba kuwalazimisha watoto wakike kuolewa ili wao wapate  fedha.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao huo,Lilian Kimati alisema lengo la Caravan hiyo ni kupita katika mikoa minne ambayo ina asilimia kubwa ya ndoa za utotoni ikiwemo mkoa wa  Mara ,Shinyanga,Tabora pamoja na Dodoma.

“Mtandao wao ulianzishwa mwaka 2012 na kipindi hicho kulikuwa na changamoto kubwa ya ndoa za utotoni hivyo walijiunga kwa lengo la kuwa na sauti moja ili kutokomeza ndoa hizo za utotoni ambapo  ulianzishwa na mashirika 12 ila kwa sasa mtandao unamashirika 87 ambayo unafanya kazi Tanzania nzima na Zanzibar,”alisema

Alisema lengo la caravan hiyo ni kupita katika mikoa ambayo inaasilimia kubwa ya ndoa za utotoni ambapo kwa sasa ni awamu ya pili  lengo ni  kuzungumza na wasichana na kuwapa elimu za masuala ya ndoa

za utotoni na  jinsi gani wazazi wanatakiwa kusimama katika nafasi zao kuhakikisha mabinti hawaozeshwi mapemana kwenda shuleni ili kufanya mambo makubwa.

Alisema  miongoni mwa mashirika ambayo yameongoza katika Caravan hiyo ni pamoja na wanachama wa Mtandao huo kutoka Shirika la Msichana Initiative,Binti Makini,Medea,Plan Internationa pamoja na My Legacy.

Mwishoo

Related Posts