DIWANI ATAKA VIJANA KUSHIKAMANA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.

 

 

Na Emmanuel Massaka, Michuzi TV

DIWANI wa Kata ya Mabwepande ,Muhajirina Kassim Obama amewataka vijana kushikamana na katika kukipigania Chama Cha MApinduzi katika chaguzi mbalimbali zitazofanyika kuanzia Serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Hayo ameseyasema Obama katika Mkutano wake na Vijana wa UVCCM Tawi la Mbopo wa Zima zote na Kuwasha Kijani lililokuwa limeandaliwa na UVCCM wa Mtaa Mbopo.

Amesema vijana ni kundi kubwa ambapo Chama limewaweka mstari wa mbele kuonesha mawazo katika kujikijenga Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Obama amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Serikali yake inasaidia vijana kuweka mazingira ya kuinua vija kiuchumi.

Amesema katika Chama kuna ya Jumuiya za makundi mbalimbali katika jamii ambapo vijana ndio kundi kubwa ya kuweza kuisaidia Chama Cha Mapinduzi katika Chaguzi zitazofanyika.

Hata hivyo amesema kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Chama hakiwezi kupata ushindi bila vijana kujiandikisha hivyo muda wenu uende kutumika kujiandikisha pamoja na kupiga kura kwa viongozi ambao wameteuliwa na Chama.
Mwenyekiti wa UVCCM) Tawi la Mbopo,Amiri Ramadhan amesema mkutano huo ni kuajiri ya kujipanga katika uchaguzi zilizo mbele yao kwa Kauli ya Zima Zote Washa ya Kijani.

Amesema uchaguzi Mkuu wanakwenda na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hakuna wa kupinga kutokana mambo aliyoyafanya kwa vijana
Katibu wa UVCCM wa Tawi Mbopo,Sikujua Matambo amesema kuwa wanakwenda kushinda katika chaguzi zote kutokana na mwamko walionao.

Related Posts