Mishi, binti mrembo wa Kitanga, ndio kwanza amefunga ndoa na dereva wa malori, Musa, ambaye amekuwa akimpa zawadi mbalimbali zilizomchanganya hadi akakolea. Ghafla anamuona shosti wake, Amina akiwa na pesa nyingi anazopewa na bwana wake mpya. Mishi anatamani naye angekuwa anapata pesa nyingi kama hizo…