‘Boni Yai’ kubaki mahabusu, hatima yake Oktoba Mosi

Dar es Salaam. Serikali imekwamisha tena uamuzi wa hatima ya dhamana ya meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob maarufu ‘Boni Yai’ baada ya kuibua maombi mengine mapya kuwa wanataka kuwasilisha kiapo cha ziada leo Alhamisi Septemba 26, 2024.

Kutokana na maombi hayo mapya ya Serikali, mvutano mkali uliibuka baina ya mawakili wa pande zote.

Mahakama imelazimika kuahirisha tena uamuzi wa hatima ya dhamana yake hadi Oktoba 1, 2024 itakapotoa uamuzi wa maombi hayo mapya ya Serikali, hivyo ‘Boni Yai’ ataendelea kusota mahabusu tena mpaka tarehe hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts