Lukuvi akana kumtaka Samia hadi 2035

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, amekana taarifa kwamba anataka Rais Samia Suluhu Hassan, atawale hadi mwaka 2035. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari wa MwanaHALISI, Lukuvi amesema, taarifa kuwa yeye anataka rais Samia atawale baada ya kumaliza kipindi chake kwa mujibu wa Katiba, hazina ukweli wowote.

“Siyo kweli. Sijasema kokote maneno hayo. Mimi nafahamu Katiba. Ninajua taratibu. Siwezi kuzungumza maneno hayo,” amefafanua.

Kauli ya Lukuvi imetokana na taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la MwanaHALISI la Alhamisi wiki hii, lililoeleza kuwa waziri huyo mwandamizi, ameonekana kwenye video akisema, rais Samia aongoze hadi mwaka 2035.

MwanaHALISI Online limeona video inayomuonyesha Lukuvi akizungumzia jambo hilo, lakini baada ya uchunguzi wake imeonyesha kuna kila dalili kuwa imehaririwa kwa nia mbaya.

Kutokana na habari hiyo, tunamuomba radhi Waziri Lukuvi kwa usumbufu alioupata kutokana na habari hiyo.

Tutazidisha zaidi umakini katika taarifa tunazozipata kupitia vyanzo mbalimbali.

Mhariri.

About The Author

Related Posts