KANALI WA GUINEA ALIYETOWEKA APATIKANA AKIWA AMEFARIKI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mwili wa Kanali wa Guinea ambaye alitoweka karibu mwaka mmoja uliopita uliwasilishwa jana kwa mkewe katika mji mkuu wa Conakry, mmoja wa Wanasheria wao alisema.

 

 

 

Kanali Celestin Bilivogui ni afisa wa pili wa Kijeshi katika miezi ya hivi karibuni kutangazwa kufariki katika Mazingira ya kutatanisha baada ya kukamatwa chini ya utawala wa kijeshi.

 

 

Mawakili wa Bilivogui walisema alichukuliwa na vikosi vya usalama kutoka ofisi yake katika idara ya pensheni ya kijeshi mapema Novemba mwaka jana kabla ya kuhamishwa kusikojulikana.

 

 

Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya Mtawala wa zamani Moussa Dadis Camara na wengine watatu waliokuwa wakishtakiwa kwa mauaji ya mwaka 2009 kutoroka Gerezani katika mji mkuu.

 

 

Siku ya Jumatano, mke wake aliitwa katika kituo kikuu cha utawala wa kijeshi huko Conakry na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti “ambapo alikabidhiwa mwili wa mumewe”, mmoja wa wanasheria wao, Salifou Beavogui, alisema katika ujumbe uliopitishwa kwa vyombo vya habari.

Related Posts